Angalia na macho ya mtoto
'Watoto wadogo waweza kupatia maana mengi'
Tukifaulu watoto wetu zaidi, tunaweza kuwasaidia na kuwapatia maoni bora. Jinsi mmoja tunaweza kufanya hivi ni kufikiria juu ya makumbuko ya utoto wetu na kuwaza dunia vile mtoto anaitambua.
Kumbuka vile ilikuwa wakati ulikuwa mtoto...
Fikiria juu ya mambo muhimu uliopitia ukiwa mtoto na pia fikiria juu ya vile mambo haya yameathiri maisha na mahusiano yako.
Wazazi wako walisema au walifanya nini ambacho ni muhimu kwako?
Ni nini ulitaka wazazi wako kusema au kufanya?
Unataka mtoto yako kukumbuka nini?
Jinsi watoto wanafikiria ni tofauti na watu wazima. Watoto hawaelewi hali vile watu wazima wanaielewa. Kwa mfano, watoto waweza kujishtaki kwa vitendo ambavyo hawakutenda.
Jaribu kutembea kwa viatu vya mtoto yako kwa saa kidogo na jaribu kumaizi vile anaona dunia. Unasikia aje kuona wewe ni mdogo vile na wote wengine ni wakubwa sana? Unasikia aje ukitaka kutambua maoni yako na unashindwa?
Watu wazima, ni wajibu wetu w kuheshimu na kushukuru watoto.
- Ongea na watoto juu ya mambo yanawahusu. Ni muhimu watu wazima wajaribu kukubali dhamira ya mtoto na pia kuhakikisha vile anafanya ni salaam na bila hatari. Watoto wakianza kuwa wakubwa, jaribu kuwaachia kukata shauri juu ya maisha yao. Patia mtoto yako hiari na kuwa tayari kukubali hiari yake.
- Saidia mtoto kuchagua na kuchukua daraka.
- Jaribu kuelewa kwamba watoto wanafikiria na wanasikia tofauti na wewe.
- Hakikisha kwamba watoto wanaona kama wazima wanawasikia. Watoto wanahitaji wazima kuwaheshimu ili wajisikie salaam.
- Shukuru na adhimisha moyo yao.
- Hakikisha watoto wako salaama na wanahifadhiwa vizuri.
Watoto wanakuhitaji kuwasaidia kukuwa na kuendelea.