Kujifahamu wewe kama mzazi
Sote tunataka kuwa wazazi bora zaidi.
Sote huwa twaanza kama wazazi wenye mbinu nyingi za uzazi.
Kila mmoja huwa na ndoto nzuri juu ya familia yake, lakini wakati mwingine mambo huenda vibaya ukajipata ukifanya mambo yeye hukusudia kufanya bila kujua imetendeka vipi.
Kama watoto wetu, maisha tunayoishi ndio yanayoonyesha hali ya maisha yetu, tunapata mbinu kuhusu watoto na uzazi kwa njia nyingi miongoni mwetu ikiwa ni pamoja na wazazi wetu, familia, marafiki, vituo vya kutunza watoto, shuleni, watalaamu na hata vituo vya habari.
Kama wazazi, mara kwa mara twapenda kufanya mambo tunayojua vizuri. Mambo hayo sana sana hutokana na maisha uliolelewa nayo ama mazingira uliokulia ambayo hutoa mchango mkumbwa kwa hisia zetu kwa watoto, uzazi na hata familia.
Kufanya mambo kinyume na matarajio
Wazazi hujipata wakati mwingine wakifanya mambo ama kusema mambo wasiotarajia.
“Sipendi kuwafokea watoto wangu, lakini hunipandisha hasira mpaka siwezi kujizuia”.
Mara kwa mara, wakati kama huo mzazi hujihisi anashukisha hadhi ya familia yake.
Wakati mwingine mzazi hukabiliana na hali hii vizuri sana, na hii huwa ni kwa sababu ya kuelewa chanzo cha hisia hizo, basi kurahisisha jinsi ya kukabiliana na watoto vizuri.
Kujijua wewe na mtoto
Watoto hutupa changamoto na kutufanya tuwe wachangamfu katika uendeshaji wa tabia na hisia zetu. Unaweza kupoteza uwezo wa kukabiliana na mambo haya ikiwa una mawazo mengi,umechoka, una hasira au kuudhika.
Hisia na matakwa yetu yanaweza kuleta hali ambayo haikutarajiwa na kuwacha mzazi na mtoto katika hali ya mgongano na kutoelewana.
Kama mzazi ni vizuri kujua jambo linaloweza kupandisha hasira zetu. Wakati mwingi watoto hufanya mambo ya kutupandisha hamaki na kujikuta uhusiano baina yako na mtoto umeharibika. Basi ni vizuri kujaribu kutenganisha matakwa na hisia zetu kando na hali ile ya mtoto ili kuwe na maridhiano mazuri.
Ingawa kujiangalia wewe mwenyewe inakufanya ujue ni kwa nini tunafikiria au kufanya vile tunavyofanya, pia inakuwezesha uwe mchangamfu na mzoefu katika kazi ya uzazi.
Ni wapi mbinu hizi za uzazi hutoka?
Ni wapi matarajio kuhusu mtoto hutoka?
Ni vipi utoto wako mwenyewe unaathiri uzazi wako leo?
Nini napenda juu ya uzazi wangu?
Nini mtoto anahitaji kutoka kwangu ambayo ni tofauti na ile niloyohitaji kutoka kwa wazazi wangu?
Nini ninastahili kubandilisha katika uzazi wangu wakati mtoto anapozidi kukua?