Kuelewa hisia za mtoto kadri anavyokuwa

Tunapoongea kuhusu hisia kadri mtoto anavyokua tunaangalia uwezo wa mtoto:

  • Kuelewa na kujua hisia zake.
  • Kuangalia kwa makini na kuelewa hisia za wenzake.
  • Kuwa na uwezo wa kukabiliana na hisia zake.
  • Kuweza kuamua tabia yake.
  • Kuelewa na kuhisi matatizo ya wenzake.
  • Kuwa na uhusiano nzuri na marafiki, familia na wengineo.

Toka watoto anapozaliwa, huwa ni wepesi wa kukuwa kimawazo na uwezo wa kukabiliana na hali tofauti za hisia.

Kukabiliana na Hisia

Uwezo wa mtoto kukabiliana na hisia ni jambo la muhimu katika maisha ya utotoni, hivyo basi kuhitaji uwepo wa mzazi.

Mtoto anapozaliwa bado huwa hana uwezo  wa kukabliliana na hisia zake, ni rahisi kwa mtoto kuzidiwa na hisia na kutoweza kujituliza, hivyo basi anahitaji mwongozo wa mzazi. Ni rahisi watoto kuwa na hasira kwa sababu wangependa kufanya jambo fulani lakini hawawezi kulifanya hadi kiwango fulani.

Hisia na tabia zinalingana, kukosa kukabiliana na hisia kwa nji bora, inaweza kuaadhiri uwezo wa mtoto wa kufikiria na kufanya mtoto kukabiliana na hisia zake bila kufikiria.

Wakati mtoto anopoanza shule, tayari huwa na uwezo wa kuelewa hisia zake na tabia za wenzake. Pia huwa na uwezo wa kulinganisha mawazo na hisia kwa kutumia maneno. Hivyo basi kuwa na uwezo wa kubadilisha na kurekebisha hisia zao. Watoto wana uwezo wa kubadilisha na kuzoea hisia zao na kuwa na hali nzuri ya kukabiliana na changamoto vyema, na kuweza kujituliza vizuri.

Uhusiano ni muhimu katika hisia za watoto

Jinsi wazazi wanavyokabiliana na watoto ni muhimu sana katika hisia za mtoto. Uhusiano kati ya mzazi na watoto huwa na adhari katika hisia za mtoto.

Watoto huwa na uwezo wa kukabiliana na hisia kwa kuangalia jinsi watu wa familia wanavyokabiliana na hisia zao. Mzazi huwa kiungo muhimu kwa kumpa mtoto mbinu za kukabiliana na hisia mzito.

Watoto wanahitaji usaidizi na mazoezi katika kukabiliana na hisia zao.

Kusaidia kujenga hisia za mtoto.

Weka mazingira ya nyumba kuwa tulivu na yakuridhisha.

Kubali hisia za mtoto na kuzishugulikia.

Wasomee hadithi zenye hisia tofauti, hii inasaidia mtoto kuelewa zaidi kuhusu hisia zake mwenyewe.

Fundisha mtoto kujieleza kwa kutumia maneno. Mfano, “yaonekana kama huna raha”.

Jaribu kujua hali zinazofanya mtoto kuwa na wasiwasi, raha, hasira au hofu.

Msifu mtoto anapokuwa mtulivu na tabia njema.

Fundisha mtoto kujua tofauti ya hisia na maadili. Mfano, wakati mto amepandwa na hasira, unaweza kumwambia “Najua una hasira lakina sio vizuri kutoa hizo hasira”.

Fundisha mtoto kujua tofauti ya hisia zake na za watu wengine. Mfano, wakati amehuzunika unaweza kumwambia ‘Hivi sasa najua una huzuni lakini unachokifanya kitasababisha dada zako kuwa na huzuni.