Kila mtoto ni tofauti
Hali ya kutofautisha ama kuwalinganisha watoto wako na watoto wengine huwa ni hali ya kufarahisha sana kwa wazazi;- lakini pia inaweza kuwa ya kutia wasiwasi kuwa kuna kasoro fulani na mtoto wako ama kuna kitu unafanya ambacho sio sawa kama mzazi.
Watoto hukua katika hali na wakati tofauti
Watoto hukua kwa viwango tofauti na kukumbana na mambo mengi wanapokua, ni kawaida kwa watoto kukumbana na changamoto za utotoni wanapokua.Watoto wengine ni wepesi kujua mambo na wengine huchukua muda.Hii ni hali ya kawaida kwawatoto wanapopevuka na miwishowe huweza kujimundu.
Watoto wana vipawa kwa uwezo tofauti, wengine ni wazuri kwa michezo, wengine kwa miziki, wengine ni wazuri katika kusoma, wengine huwa wenye wasiwasi sana na wengine wenyekutulia, wengine waweza kulala vizuri na wengine wanaamka kila mara usingizini kwa miaka.
Kuhisi kujiamini kwamba uko kwenye mwelekeo unaofaa
Wazazi wengi hukabiliwa na changamoto za uzazi na kushindwa ni vipi wanaweza kuwa wazazi bora na hutatizwa na jinsi watakavyo kuza watoto wao ili wafaulu shuleni, kwenye michezo na hata kazini.
Wengi huhisi kuwa uzazi sio kitu rahisi.
Wazazi wengi hujihisi kuwa hawapati mahitaji kamili ya watoto wao hivyo basi hujiona kama kwamba wanasemwa vibaya na wenzao.Hali hii hufanya mzazi kujikuta katika hali ya upweke, kujitenga na wengine na kujiona kuwa hali hii inamkumba yeye peke yake.
Hauko peke yako
Kazi ya uzazi heuendelea kubadilika kulingana na jinsi watoto wanvyozidi kukua, hivyo basi, anachohitaji mtoto mwingine ni tofauti na mwingine.Hali ilivyokuwa wakati wakiwa miaka miwili sivyo itakavyokuwa wakiwa miaka minne.
Kuzoea na kuwa na urahisi wa kuingiliana na hali inapobadiliki ndio jambo muhimu katika uzazi.
Unapokosa kuwa na imani katika kazi ya uzazi ni vizuri kuchangia mawazo na wazazi wenzako, familia au marafiki na kuzungumza hali hii pamoja. Utajikuta kuwa hauko peke yako Kutangamana na wengine itakusaidia kujua iwapo unatenda mambo yako sawa sawa na pia inakupa imaini zaidi.
Amini kuwa unamjua mtoto wako vizuri kuliko mwingine yeyote.
Epuka kulinganisha au kufananisha mtoto wako na wengine.
Ikiwa una wasiwasi kuhusu mtoto wako pata ushauri wa mtaalamu, ni sawa kutafuta usaidizi wa mtalaamu, hii ni dalili yaushujaa na wala sio kuonyesha unyonge.