Elewa mwanako anavyozungumuza
Kumfikisha mtoto mchanga nyumbani yaweza kuleta furaha na hofu kwa mtoto na kwa wazazi pia.
Kazi kuu kuhusu kumtunza mtoto mchanga ni kuhakikisha kwamba mahitaji yake yamepata sululisho. Mahitaji ya watoto wachanga ni ya msingi sana: watoto wachanga hupata njaa, husikia mchoko na kukosa starehe.
Miongoni mwa vitu vinavyomleta mtoto mchanga kukosa starehe kunakuwa:
- Wakati wa joto au baridi nyingi
- Akihitaji nepi ibadilishwe
- Akiwa anaumwa (maumivu ya sikio au ya tumbo), kuhusu watoto wakuinukia hii yaweza kuwa maumivu ya meno
- Anaposhitushwa, akiwa mwenyewe au akichoka
- Asipojisikia vizuri (pengine akiwa na homa nyingi)
Watoto wachanga wanakuwa na njia nyingi za kuvutia uangalifu wa wazazi wao na kuwasiliana nao kwa kuwawaelezea mahitaji yao. Wazazi hujifunza, baada ya mda, maana ya ishara hizo na jinsi ya kuzisuluhisha. Mwanzoni, ni vyepesi kutokutambua au kutafsiri vizuri alama hizo. Ni baada ya muda fulani ndipo ishara hizo huanza kutafsirika na kueleweka.
Kwa nini mtoto mchanga hulia?
Alama kuu mtoto mchanga anayotumia kwa kuvutia uangalifu ni kulia. Haraka, mzazi hutambua kwamba mtoto hutumikisha aina mbalimbali za kulia kwa mjibu wa mahitaji yake. Watoto wanalia wahitaji kitu.
Watoto wachanga hawalii kuudhi au kusumbua wazazi wao. Watoto huisi tu, hawawezi fikiri, hawawezi kutazamia yasiokuweko bado au kutumia ujuzi wowote ule. Hawaelewi hata namna gani kilio chao kinawathiri watu wengine, wanajua tu kwamba wanahitaji kitu na kwamba kulia ndiyo njia moja tu ya kumjulisha mtu fulani wanachokihitaji. Mtoto mchanga hulia ili aweze kujinusurisha na pia ili mzazi aweze kusuluhiza tatizo lake.
Kwa jinsi unajifunza zaidi kuhusu mwanako, unagundua kwamba watoto wachanga huwasiliana pia katika njia zingine mbalimbali.
Kutazama mtoto kwenye uso huonyesha namna zingine tofauti watoto wachanga wanazozitumia kwa kuwasiliana na watu. Wazazi hujifunza alama hizo na kuzielewa na kutambua mahitaji ya mtoto kabla hajalia. Nyuso za watoto wachanga zinaeleza waziwazi, wanakuwa na uzoefu wakutia mistari ya wasiwasi juu ya pua yao, ambayo kwa watoto wachache ni kitambulisho kionyeshacho kwamba mtoto anataka nepi ibadilishwe. Pia, vinywa vya watoto wachanga hueleza mengi; watoto hukunja midomo na hutumia ndini zao kwa kuwasiliana.
Pamoja na ile, watoto hutumia mikono yao, zaidi konde (ngumi), kutambulisha kwamba wanahitaji kitu. Wazazi wanaelewa kufunga konde kuwa pengine ni alama ya kukosa starehe, au ya kusikia njaa. Watoto pia hutumia viungo vingine vya mwili wao kutahazarisha wazazi kuhusu mahitaji yao, mara hukunja mgongo na kutupatupa miguu yao.
Kuwasiliana na mwanao
Kama vile watoto wanavyowasiliana nasi, tunahitaji pia kuwasiliana nao. Utafiti umetahazarisha wazazi kuhusu umhimu wa mawasiliano, wakuchekea na wa kusomea mtoto. Mara kwa mara wazazi wamefikiri kwamba kuwasiliana na mtoto mchanga ni kupungukiwa kiakili kwani mtoto huyo hawezi jibia kwa kunena. Lakini mtoto anakuwa akijibu, na kama vile wazazi hufafanua ishara na kuelewa mahitaji ya wanao, kadhalika mtoto hutumia ishara kwa kujibu na kama njia ya kuwasiliana.
Watoto wanaosemeshwa au wanaosomewa kuwa wakikazia macho anayezungumza, wataweza kucheka sana au wanatoa sauti nyingine au kuwasiliana kwa kutumia mikono (hapana kufunga konde), lakini akiachanisha vidole na anaweza kushika au kucheza na nyao za miguu.
Watoto wachanga hufurahia vitu vizuri, vinavyovutia macho na pia wanafahamisha furaha yao kupitia uso wala viungo vingine vya mwili. Hali hii ya kubadili alama za mawasiliano kati ya mzazi na mtoto hua chanzo cha uhusiano wa tunzo na pendo, ambayo mtoto na mzazi wafurahia.
Kugusa ni nyingine ishara mhimu ya mawasiliano kati ya mtoto na mzazi. Wazazi waweza kujifunza kuchuliwa watoto wao na kujifunza matakwa ya wanao, wakiangalia wananvyozun gumza kupitia viungo vya mwili wao. Kugusa ya upendo katika hali ya kutunza mtoto kama vile kumukumbatia, kumshika mikononi na njia zingine za kumubembeleza mtoto, zaidi kwa kumtuliza, ni njia mhimu ya mawasiliano yenye kuzidisha upendo na ushirika kati ya mzazi na mtoto.