Kukabiliana na ungomvi katika uzazi

Familia nyingi hukumbana na mambo yenye uwezo wakuleta rabsha kati ya wazazi. Wakati mwingine uzazi ndio huwa chanzo cha fujo baina ya wazazi. Kutokubaliana kwingine hakuwezi kuepukana katika familia yeyote, hivyo basi ni vizuri kujifunza jinsi ya kukabiliana na hali hiyo.

Jinsi wazazi wanyosuhulisha migongano yao inaweza kuadhiri watoto wao. Watoto hujihisi kuwa bila wasiwasi na wenye salama kulingana na uhusiano wa wazazi wao.

Watoto hujifunza na matendo ya wazazi wao

Wazazi wakiwa wanaendelea vizuri, uhusiano baina yao humsadia mtoto kujua jinsi atavyoweza kukabiliana na wenzake. Watoto wanaweza kusuhulisha migongano baina yao iwapo wamezoea kuona wazazi wakikosana na kisha kusuhulisha mgongano huo kwa njia nzuri.

Migongano ya mara kwa mara baina ya wazazi ina madhara katika mtoto kwasababu watoto wana uwezo wa kuhisi kuwa kuna mgongano baina ya wazazi wao hata kama hawaoni mkigombana.

Watoto wengine hukabiliana na hali hii kirahisi lakini wengine hushindwa. Hii nikutokana na uhusiano wa mtoto na watu wengine kwenye familia wanaomsadia kwa kumpa wasia mzuri, mfano wasia mzuri kutoka kwa nyanya au babu yake.

Migongano baina ya wazazi inaweza kuwa na adhari kubwa sana kwa watoto na kuwafanya wawe na tabia tofauti tofauti na kuadhiri jinsi wanavyohusiana na jamii, pia kuadhiri jinsi wanavyoendelea kukuwa. Mtoto pia anaweza kuwa na shida ya kukosa raha, kuwa na wasiwasi, haya, hasira na ujeuri, shida ya kukosa usingizi na kushindwa kuelewana vizuri na marafiki.

Suluhisho

Epukana na kuzozana mbele ya watoto.

Usiweka watoto katika hali ya kuwafanya kuamua ama kuchagua upande mmoja wa wazazi (upande wa baba au wa mama).

Usiwatumie watoto kama kisingizo cha kufikia matakwa yako.

Mjifunze kujadili tofauti zenu kwa utaratibu.

Waeleza watoto kuwa wao sio chanzo cha migongano yenu.

Waonyeshe watoto kuwa unawependa na mnasuhulisha migongano yenu.

Kuwa na muda wa kuwasikiliza watoto jinsi wanavyohisi hali hii ya mgongano.

Kila mmoja kuheshimu mawazo ya mwingine hata kama kila moja ana mawazo tofauti na mwenzake.

Ni vizuri wazazi kuwa kama kitu kimoja hata kama kuna tofauti Fulani baina yao. Tembelea mtaalamu ikiwa hali hii inazidi kudorora na kuadhiri watoto wako na uhusiano wako.