Familia madhubuti na zenye furaha
Familia madhabuti na zenye furaha huumba hali nzuri katikati ya jamaa na kwa kila mtu aliyemo. Katika uwepo huo mzuri hupatikana afya ya mtu kimwili, kiakili, kihisia na kijamii. Familia madhabuti na heri huhimizana na kuchukuliana ili kila mmoja awe imara, awe mwenye tumaini na hupiganisha pamoja kwa kutimiza lengo kwa kila mwanamemba kibinafsi na kwa jamaa lote kwa jumla. Katika familia madhabuti na zenye furaha, kila mtu anakuwa na haki ya kujisikia salama, mwenye starehe, mwenye furaha na mwenye kupendwa. Wazazi wanalo jukumu la kuwa vielelezo kwa watoto wao na kuwatia katika mazingira yenye malisho mazuri ili waweze kufanikisha maisha yao.
Mradi wa Utafiti kuhusu Nguvu za Jamaa (The Family Strengths Research Project) limetambulisha aina nane za nguvu ambazo familia madhubuti na heri nchini Australia zinakuwazo kwa jumla. Nazo ni hizi:
Uhusiano:
Familia madhubuti na heri huthamanisha uhusiano wazi, wenye njia mbili. Hii humaanisha kwamba wazazi na wanao wahakikishe kuwa kila mmoja husikiliza mwenziye na kupeana nafasi ya kusema. Familia hizi zinafungua milango kwa jamaa lote kushiri katika majadiliano kuhusu hali ya mambo ya kila siku pamoja na mida ya kujadiliana kuhusu shida na matatizo mbalimbali.
Umoja:
Kuwa umoja unakuwa kama “gundi” ili kusaidia familia kuendelesha hali ya kujiona kuwa wamoja wa jamaa hio. Hali ya umoja ni kuchangia vitu vya kufanana kama vile thamani, imani au tabia. Watoto wanaonekana kuwa kama wana familia wakiwa wenye uthabiti madhubuti kwa kuwa kwenye jamaa hio. Familia madhubuti na yenye furaha hufungwa pamoja katika safari ya maisha.
Kuchangia shuguli:
Familia madhubuti na heri huchangia na kufanya vitu vyote pamoja. Inaweza kuwa michezo mbalimbali, kusoma hadithi, kuwa na mda wa pamoja, kuchangia wanavyovipendelea pamoja na likizo. Jinsi watoto wanavyokomaa, kuwaza zaidi kibuni huitajika kwa kuwajumuisha katika shuguli za jamaa. Mapendekezo huhusika na kualika rafiki za watoto wakubwa kujiunga katika shuguli za familia na kuunda nyumba ya vijana rafiki kwenye rafiki za watoto huhimizwa kiuhai na kwenye wanaweza kupitisha mda mwingi pamoja.
Upendo:
Upendo hujidhihirisha katika shirikisho safi la hisia katika hali ya kukumbatiana na katika mabusu. Familia madhubuti na zenye furaha huelezeana jinsi wanajisikia, hufikiria kila mtu juu ya mwenziye na kushugulikiana, huhusishiana na kufurahiana.
Kusaidiana:
Kila mwanamemba wa jamaa madhubuti na heri anajua kwamba wanamemba wengine wa familia watakuwa hapo daima kwa kumtakia mema. Katika jamaa za namna hii, ni vema kuomba msaada na kuhimizwa.
Hali ya Kukubaliana:
Wanamemba wa familia madhubuti na zenye furaha huwa na hali ya kuheshimiana na tathmini ya utofauti wa kila mmoja. Mashindano yanapigwa marufuku na wanamemba wa jamaa hukubaliana na huthamanisha hali ya kila mmoja kuwa jinsi alivyo tofauti na mwengine yeyote. Wanaheshimu maoni ya wengine, wanasameheana na kukubaliana kila mmoja kuenenda sawasawa na nguvu zake.
Ahadi:
Familia madhubuti na heri zimejiweka wakfu na uaminifu kwa kila mmoja binafsi na kwa jamaa yote kwa jumla. Familia hizi zinajisikia kuwa salama na tulivu pamoja na kila mmoja, zinaaminiana na kutimizia ahadi.
Uelezi:
Jamaa madhubuti na heri zina uwezo wa kujifunza kwenye mazingira yenye kubadilika na kuwa na mtazamo wa hakika kuhusu pinzani ziwezazo kutokea. Familia madhubuti na zenye furaha huzungumzia vitu kwa ndani, huhimiza kila mmoja wao kuhusu mipango yake, husaidiana wote katika hali ngumu, hujifunza kama familia kwa namna wanavyoenenda. Katika familia madhubuti na heri, mahusiano kati ya watu wazima na watoto ni yenye kukomalisha na kusaidia, karimu na ya haki, ambamo watoto huwa na hali madhubuti ya umhimu na ya kuwa wamoja wa familia.