Kumfahamu mtoto

Ni vizuri kujua mtoto anavyohisi ama anataka nini. Kufahamu mtoto kwa hali hii inarahisisha uhusiano baina ya mzazi na mtoto. Mzazi mwenye kujali hufanya mtoto wake kujua kwamba anamjali na mahitaji yake yanashugulikiwa.

Watoto wana uwezo wa kujua kama mzazi anawajali au la. Hali hii hujenga sana uhusiano kati ya mzazi na mtoto anopozidi kukua

.

Ukiwa unamfahamu mtoto unakuwa kwenye hali nzuri ya kujua mienendo na tabia zake na hata kujua jinsi ya kukabiliana nazo. Wakati mtoto anapofahamu kuwa anashugulikiwa vyema huwa katika hali ya kujiamini na mwenye kuridhika.

Mtoto anapozaliwa huwa na njia zao za kutoa ujumbe kupitia sauti.kama vile kulia, kutabasamu, kurusha miguu akiwa na raha ama akiwa hana raha. Kumfahamu mtoto wako huanzia mtoto hajaanza kuongea na kuwasiliana kupitia ishara ama vitendo kama kuangalia macho yake,ishara za usoni, sauti yako na kutumia vitendo kuwasiliana.

Mtoto anapoendelea kukua inakuwa rahisi kumfahamu kupitia vitendo na hata kuongea nae.

Kuendelea kumjua mtoto

Kumfahamu mtoto ni muhimu sana kwani mtoto hujihisi kuwa yuko salama na mwenye kupendwa. Mtoto anapolia unatakiwa ujue iwapo anahisi njaa, amechoka, anataka umkubatie ama anataka kubadilishwa napi.

Kumfahamu mtoto mchanga inakuwa rahisi kujua ni wakati gani hataki kelele, anataka kula, ama anataka kufanya kitu tofauti. Kumuelewa mtoto wa miaka miwili ambaye yuko katika hali hasira na kutoulia, inatakiwa umbakabili kwa njia nzuri na pia kuelewe kinacho sababisha hali hiyo, je amechoka? ame ameumia?.

Kuweza kumfahamu mtoto inahitaji subira na uvumulivu ndipo uweze kumjua vizuri.

kufamu kinachoendelea

Kumbuka kila mtoto ni tofauti na mienendo yao na njia tofauti ya kuwasiliana.

Chunguza mtoto wako na uelewa ni kitu gani kinamfanya awe na tabia fulani ambayo ni sawa.

Zielewa na uzizoe mienendo na tabia za mtoto wako. Je utajuaje ikiwa anahisi njaa?

amechoka?anahitaji usaidizi wako? anahitaji kubembelezwa?.

Kuwa mwangalifu sana katika mabadiliko ya hali ya mtoto hasa sauti na mienenendo zao.

Jua uwezo wa mtoto wako kukabiliana na mambo. Je huonyesha nini wakati anahisi raha? Je yeye ni mtu wa kushindwa na mambo rahisi? Je yeye hunyamaza kimya wakati amekasirika? Mshuhugulikie anapokutolea ishara iwe kwa kukuangalia, kwa vitendo, au kutoa sauti.

Anapoinua mikono yake kuonyesha anataka kubebwa, muinue na kumbusu na tumia maneno kama “beba”

Ongea na mtoto wako na mpe nafasi ya kukuongelesha na umsikilize.

Heshimu na utilie maanani hisia za mtoto wako.

Hakikisha vitendo na maneno unayotumia kwa mtoto wako ni sawa na hisia zake.