Kuboresha tabia za mtoto

Mtoto hujifunza mambo mengi kuhusu ulimwengu wao na namna yakuhusiana na wenzake. Hii humwezesha mtoto kujifunza na kujipa motisha wa kujaribu vitu vipya.

Uboreshaji wa tabia huabatana na hisia za watoto. Mtoto alie na uwezo wa kukabiliana na hisia zake kama hasira au mshutuko ana uwezo mkubwa wa kucheza na watoto wenzake na hata kusuhulisha mgongano unapotokea baina yao. Kadhalika mtoto anaye elewa hisia za wenzake ana uwezo mkubwa wa kukabiliana na mahitaji ya watoto wenzake wanapocheza.

Wewe kama mzazi ni kiungo muhimu katika kuunganisha mtoto wako na watoto wengine.

Mtoto hujifunza uhusiano kulingana na vile wewe mzazi unakabiliana naye na pia vile unavyo kabiliana na watu wengine.

Watoto hupitia hatua nyingi za kitabia, na hapo ndipo anapopata mbinu nyingi za kitabia, sana sana kupitia michezo na miigizo. Jinsi mtoto anavyocheza huenda ikabadilika kulingana na umri. Anavyozidi kukuwa huwacha kucheza peke yake na kuanza kufuata wenzake na baadaye kujiunga nao kikamilifu.

Mjue mtoto wako

Watoto wako na umri tofauti na kutoka kwenye mazingira tofauti, hivyo basi wao hukabiliana na mbinu tofauti ya kukabiliana na tabia zao. Watoto wengine wana haya, wengine hupata marafiki kirahisi, wengine huwa na hali ngumu wa kupata marafiki, wengine huweza kuelewana na wenzake kirahisi lakini wengine hawawezi.

Mchunguze mtoto kwa mazingira tofauti tofauti, angalia ni vipi anavyo kabiliana na hali hizo, je yeye hubadilika kulingana na kubadilika kwa mazingira? Je yeye ni mchangamfu wa kukabiliana na hali hii? Je, anahitaji usaidizi wowote? je, ni hali gani yeye hukabiliana nayo kirahisi? na pia ni jambo gani au hali ipi huwa ngumu kwake?.

Kama vile kujifunza kutembea na kuongea, mtoto pia anahitaji mbinu za kitabia kutoka kwa mzazi, ni wajibu wako kama mzazi kuhakikisha mbinu hizi anazifanyia mazoezi mara kwa mara ili kusizoea.

Njia za kumsaidia mtoto

Andalia mtoto mazingira mazuri nyumbani, na pia kumzoesha hali ya kuwahusisha wenzake Unda zile tabia unazohitaji mtoto kuwa nazo na kuhakikisha ndungu zake wakumbwa wanakuwa mfano mzuri kwa wale wadogo.

Wafundishe kusaidia katika kazi za kila siku nyumbani na pia kubali wanapojitolea kukusaidia. Mzoeshe mtoto jinsi ya kukabiliana na wenzake wakubwa kwa wadogo kwa kuwa na huhusiano inayokubalika.

Msaidie mtoto kuwa na motisha wa kimaisha. Hali hii ni muhimu sana kwa uboreshaji wa uhusiano wake na jamii.

Msaidie mtoto kuelewa hisia zake na hisia za watoto wengine.

Msaidie mtoto kujua mbinu za kujiunga na wenzake hasa makundi na jinsi ya kufuata sheria na kujua wakati wake kuchangia.

Watoto wengine hawapendi vifaa vyao vya mchezo kutumika na watoto wengine, hivyo basi huwa vigumu watoto hawa kuwaruhusu wenzake kucheza na doli au vifaa wapendao zaidi.

Weka kando vifaa hivi wakati watoto wanapocheza na marafiki.

Wape watoto fursa zaidi ya kucheza na wenzake.

Wajue marafiki ambao watoto wako hucheza nao shuleni na kuwaalika ili wacheza pamoja.

Tenge siku za kucheza kwa pamoja kwa wale wachanga na kuwaandalia michezo isiokuwa na muda mrefu na ambazo watafurahia. Pole pole waongezee muda wa kucheza, idadi ya marafiki na punguza jinsi unavyopanga michezo yao maanake watoto wanavyozidi kukua hupata ujuzi wa kuzoea na kukabiliana na hali hii vizuri.