Changamoto katika uzazi
Wazazi wengi hujikuta wakinga’nga’na kukabiliana na hali ya kimazingira wanapolea watoto wao.
Wengine huwa na wasiwasi wa usalama wa watoto wao.
Wazazi wengi huhisi kuwa watoto wanaingilia mambo ya kiutu uzima mapema kabla ya umri wao.
Wazazi wengi huwa wanajipata katika hali ngumu ya kukabiliana na shughuli za kazini na za uzazi.
Wengi hujikuta kwa upweke kwa kukosa nafasi ya kukutana na watu wa familia na marafiki.
Changamoto zinazokumba wazazi wa leo ni dalili wazi kuwa wanajitahidi sana hivyo basi huleta uchovu wa akili.
Hauko peke yako, wazazi wengi wanakumbana na hali hii kama wewe
Uchovu wa akili ni jambo la kawaida katika uzazi, uchovu kidogo sio mbaya mradi unaweza kuendelea na kazi zako za kawaida. Lakini uchovu mwingi wa akili inaweza kukufanya uwe katika hali ya kushindwa kujishughulikia na kuwa muoga wa kufanya mambo.
Hakuna mzazi bora zaidi kwa kuwa mara kwa mara huwa twashindwa kukabiliana na mahitaji ya familia vilivyo. Jambo muhimu ni kujaribu kujua ni wakati gani tumezidiwa na fikira na kutafuta njia ya kukabiliana na hali hii.
Kujishughulikia wewe na kutakufanya utunze watoto pia
Usiwe mtu wa kuweka wengine mwanzo kila mara na kujisahau. .
Fanya mambo ya kukuwezesha kutulia kama vile kusikiza muziki,kusoma vitabu ama kufanya matembezi hata kama ni kwa dakika kumi.
Angalia jambo linalosababisha kuwa na fikira nyingi na ulishughulikie vilivyo kwa hatua unayoweza.
Unda ratiba ambazo mtazifuata kikamilifu wewe pamoja na watoto.
Angalia jambo ambalo ni muhimu sana kwako na familia yako.
Jipe ruhusa ya kutokuwa kamilifu sana.
Epuka kutoa hasira yako kwa watoto. Wakati unapotamka jambo ambalo sio nzuri mbele ya watoto ni vizuri kuwaomba msamaha na kukubali kosa lako.
Jitengee wakati wako spesheli na pia wa familia.
Jaribu kuzungumzia mambo yanayokutatiza na mme/mke mpenzi wako, rafiki au mtu wa familia, kupitia mazungumzo haya huenda ukapata afueni na kujinusuru katika upweke.