Je siku hizi nimekuambia nakupenda
Kile tumechoambiwa na wazazi wetu kitakaa nasi kwa milele.
Watoto wanatakiwa kusikia kama wanapendwa na kukubaliwa vile wameumbwa, sio kwa ajili ya mambo wametenda vizuri au kazi wamefanya.
Kila mtoto ni tofauti ni pekee
Thamini na shajiisha tofauti za kipekee za watoto.
Kila mtoto ana vitu vingi vya kuchangia kwenye familia, warafiki na jamuia.
Watoto wanatakiwa kujisikia vizuri
Kujiheshimu ni kusikia vizuri ukifikiria juu yako, na kujisikia kama uko azizi. Kujiheshimu hupatia mtoto imani na thamani kwa wakati wa mbeleni. Watoto wanatakiwa kujipenda, kusikia kama wako muhimu, welevu na wanaweza kutekeleza mengi maishani mwao. Watoto ambao wanajiheshimu wako na tumaini kwa kujifunza na kujaribu kufanya mambo mapya.
Jinsi ya kuwambia watoto umuhimu wao
Wambie mara nyingi unawapenda vile wameumbwa.
Unaweza kuwaonyesha unawapenda ukitoa wakati wa kushinda nao, ukisikia maneno yao na kukumbatiana nao na kucheka nao.
Sherekea matekelezo yao, hata kama ni ndogo.
Wasifie kwa kujaribu, usilinganishe matokeo ya kile wanachofanya.
Weka makumbusho spesheli ya mafanikio na hatua yao.
Wakitaka kukusaidia wapatie nafasi.
Wajulishe ni sawa kufanya makosa. Kile wanachofanya kinawasaidia kujifunza.
Wasaidie kujenga vipaji vyao.
Waulize fikira zao juu ya mambo yanayofanyika kwa jamii. Hii itawaonyesha unajali vile wanafikiria.
Wasaidie kusululisha matatizo yao. Waonyeshe uko na imani nao.
Linganisha na bainisha mifikio na matarajio yako.
Watolee marudio juu ya miendo yao ambaye sio sawa lakini usiwahukumu.
Dhamira ya marudio ni kufundisha mtoto wako sio kumumiza.