Malezi ya babu na bibi
Zaidi ya miaka thelathini iliyopita, picha ya babu/bibi pamoja na kazi yao ndani ya jamaa imebadilika mno. Kazi ya babu/bibi kuhusu wajukuu wao yaweza kuwa tofauti kufuatana na hali ya jamaa. Hakuna kielelezo kamili ya kuwa babu/bibi. Huyu hujikuta katika hali ya kusaidia na hivi kujiingiza wenyewe ndani ya mambo ya watu wengeni, wala hutaka watoto kulelewa jinsi wao walivyofanya, au kuawaacha wafanye wenyewe wanavyotaka.
Mababu wamoja huishi pamoja na jamaa zao na kuchunga wajukuu wao wazazi wao wakiwa kazini. Mababu/bibi hawa hujishugulisha mno na maisha ya wajukuu wao, wakati fulani huanzisha harakati za kuhudumia wajukuu wao. Wakati hawaishi na wajukuu wao, mababu/bibi wengine pia hujitolea katika aina mbalimbali kwa kushugulikia wajukuu wao, kwa mfano, kuwapeleka shuleni na kuwarudisha nyumbani na kuwajali baada ya shule au wakiwa likizoni.
Katika jamaa zingine, mababu/bibi huwa wafanyakazi. Kwa hiyo, yawezekana wasiweze, au wasitamani kuitika huduma hiyo katika maisha ya wajukuu wao. Mababu/bibi hawa waweza kujishugulisha na hali ya kupitisha mda fulani pamoja na wajukuu wao sehemu na wakati zinazuridhisha mababu na jamaa.
Wengine waweza kutokuona wajukuu wao mara kwa mara, wala hata kuhusiana nao. Hii hutokea kwa sababu mbalimbali kama vile kuishi mbali ya jamaa zao au pengine sababu ya mafarakano ndani ya jamaa. Hali hii yaweza kuwa chanzo cha huzuni kwa mababu hao kwa kutoshiriki katika maisha ya wajukuu wao.
Leo, kwa sehemu kubwa, wababu waweza kuwa mda wote kama wazazi kwa wajukuu wao katika nyumba zao, ikiwa wazazi wao huonekana hawawezi au hawataki kuwahudumia wenyewe.
Katika hali zote, mababu ni watu wenye manufaa katika maisha ya wajukuu wao. Kwa watoto, mababu zao huwapatia kao lingine mbali na kwao, usalama, msaada na upendo usio na masharti.
- Mababu/bibi mara kwa mara hupata mda wakubakia pamoja na wajukuu wao zaidi ya wazazi wao wenye shuguli nyingi. Jaribu kupitisha mda nafasi ya burudani pamoja na mtoto wako, kwenye uwanja wa michezo, kutembea pamoja kwa mda wa kutosha na kumfundisha kuhusu ulimwengu wao.
- Mababu/bibi ni msaada maarufu kwa wajukuu. Jipe mda wa kusikiliza wajukuu wako. Waweza kuwasaidia kusuluhisha matalizo au wasiwasi zao.
- Wakati mwingine, mababu/bibi waweza kutoa pendekezo wakati wa mivutano kati ya watoto na wazazi, na hivyo kusaidia kusuluhisha matatizo. Jaribu kutokuegemea ngambo moja, lakini wasaidie wajukuu wako na wazazi wao kuelewa kila mmjo fikira za mwingine.
- Wajuku waweza kumimina hali yao mbele ya mababu/bibi zao. Wanaweza pia kuwafundisha teknolojia mpya, wakati mababu huwaelezea namna mambo yalikuwa yakiendelea kabla teknolojia nyipya wanazozitumainia zilikuwa hazijaja.
- Sherekea mafanikio ya wajukuu. Wahimize kuendelea kupima vitu vipya. Waonyeshe umaarufu wa tumaini na ujasiri. Mababu/bibi waweza kuwafanya wajukuu wao kufurahia maisha kwa kuchukuliana nao katika yote wanayoyawazia au kuona. Hali ya kuchanganikisha.