Ulezi ndani ya jamaa la kambo

Familia za kambo zimekuwa moja ya aina kawaida za jamaa.

Kila familia la kambo ni la kipekee na litafikiwa na mapinzano pamoja na zawadi. Kila jamaa la kambo huwa na mda wa mabadiliko makuu na mipangilio mipya kwa jinsi familia jipya linaungana. Wakati huo, fikira mhimu zaidi lingekuwa uhusiano kati ya watoto na wazazi wao.

Watoto wanahitaji uthabiti mpya kutoka wazazi wao na wazazi wa kambo kwamba wanaendelea kupendwa na kwamba siyo kosa lao ikiwa wazazi wameachana. Kila mzazi anaombwa kusema vizuri kuhusa mwenziwe. Wazazi wanaombwa kupitisha mda wa kutosha pamoja na watoto. Watoto wanahitaji uthabiti kwamba, iwe wataishi na mzazi au hapana, wazazi wote wawili watabakia sehemu ya maisha yao.

Wazazi wasioshi na watoto wao wanakuwa na kazi mhimu ya kufanya. Watoto waweza kukushirikisha kuhusu mambo mbalimnali wanayokutana katika jamaa hili jipya. Wazazi wanastahili kusikiliza na kusaidia watoto kwa nyakati hizo. Watoto wanahitaji uhusiano wa amani na msaada toka kwa wazazi wote wawili wanapoanza kushirikiana na wengine watu wazima wapya na watoto katika jamaa lao jipya.

Wazazi wa kambo ndani ya jamaa la kambo wanapashwa kufikiria kuhusu:

  • Kukuza au kukomalisha mahusiano pamoja na mshiriki mpya wa watoto
  • Kuwasaidia watoto katika familia hizo kushirikiana vilivyo
  • Njia za ulezi zikiwa ziko sawasawa au tofauti na kufikia makubaliano kuhusu namna ya ulezi ndani ya jamaa hili jipya.

Kujikuta katika jamaa jipya huwa kipindi kizito kwa mtoto. Mtoto aweza:

  • Kupoteza nafasi yake ndani ya familia
  • Kuombwa kuchangia chumba cha kulalia wakati alizoea kuwa na chumba chake mwenyewe
  • Kuchangia mzazi aliyekuwa anaonekana kuwa wake pekee
  • Kutamani jamaa la hapo awali lirudiane
  • Kuhama, kuacha marafiki, shule na watu wengine aliowajua na kuwazoea kama vile mzazi mwingine

Lakini, panaweza pia kuwa faida za kutosha kwa mtoto katika jamaa la kambo, sawa vile:

  • Mzazi wake hufurahia zaidi uhusiano mpya
  • Kunakuwa zaidi ya watu wazima wa kushugulia watoto, pamoja na babu zao
  • Mtoto kuwa amepata kaka na dada wapya
  • Bahati ya kuwa tena mmoja wa familia

Kuna namna nyingi wazazi na wazazi wa kambo waweza kusaidia mtoto wakati wa kubadilisha makao.

Watoto wanadhihirisha hisia zao katika mwenendo wao. Mwenendo wa watoto ukigeuka kuwa mbaya zaidi, hutambulikana kwamba watoto hawapo sawa. Kuwa angalifu kuhusu maelezo ya watoto kupitia maneno na mwenendo na kuyashika kwa makini.

Vitendo kawaida vinazoonyesha kwamba mda huu wa mpito ni mgumu kwa mtoto ni kama vile:

  • Upungufu wa maendeleo kama vile kuanzisha tena kukojoa kitandani au kuzungumza kitoto
  • Ndoto mbaya na matatizo mengine ya usingizini
  • Shida shuleni – vipimo kamili vya kitaalamu huonekana kupungua, na hali ya kutokupenda kushiriki tena shugli alizozifurahia hapo awali
  • Kugeuka mkali au hujihuzuru

Kama wazazi na wazazi wa kambo, munapaswa:

  • Kusikiliza mtoto
  • Kujitahidi kuelewa hali ya mambo kutokana na maoni ya mtoto
  • Kuhimiza watoto wote katika jamaa jipya kuzungumza kuhusu mawazo au matatizo yao
  • Kusaidia mahusiano lakini kuwaletea waendelee sawasawa na nyayo zao wenyewe.
  • Kuthibitisha mipangilio katika hali ya familia mpya yenye italeta kuwatoza dhamana watoto wote.
  • Kupangilia mda pamoja na kila mtoto binafsi
  • Kukumbusha mtoto wako kwamba unampenda na kwamba utaendelea kuwa pale kwa ajili yake.