Familia madhubuti na zenye furaha
Familia madhabuti na zenye furaha huumba hali nzuri katikati ya jamaa na kwa kila mtu aliyemo. Katika uwepo huo mzuri hupatikana afya ya mtu kimwili, kiakili, kihisia na kijamii. Familia madhabuti na heri huhimizana na kuchukuliana ili kila mmoja awe imara, awe mwenye tumaini na hupiganisha pamoja kwa kutimiza lengo kwa kila mwanamemba kibinafsi na kwa jamaa lote kwa jumla. Katika familia madhabuti na zenye furaha, kila mtu anakuwa na haki ya kujisikia salama, mwenye starehe, mwenye furaha na mwenye kupendwa. Wazazi wanalo jukumu la kuwa vielelezo kwa watoto wao na kuwatia katika mazingira yenye malisho mazuri ili waweze kufanikisha maisha yao.