Umuhimu wa uzazi katika kukuza akili ya mtoto

Akili ya binadamu inachukua muda kukua. Mpaka kuzaliwa, kwa kawaida akili inakuwa imeshakuza vitu vingi kama vile kuhema, kudunda kwa roho, kulala na pia uamuzi wa mambo. Sehemu zingine za akili huchukua miaka kukua.

Kujua jinsi akili ya mtoto inavyokuwa ni njia nzuri ya kuelewa ni nini mtoto anafikiri ama anachohisi. Watoto wachanga akili zao huwa bado ni duni hivyo basi kuwa na ugumu wa kujiamulia mambo, hii ni kwa sababu sehemu ya akili inayohusika na mambo hayo bado haijaanza kazi katika umri wa utotoni.

Kuelewa jinsi akili ya mtoto inavyokua inakupa busara kwa maswali amabayo wazazi hujiuliza mara kwa mara kama…….KWA NINI?

Kwa nini wamefanya hivyo?

Kwa nini hawasikilizi?

Kwa nini mpaka niseme jambo mara kwa mara?

Kupevuka kwa akili

Mazingira, chembe cha moyo (Jene) na kila hatua ya kupevuka kwa akili huambatana katika kazi zao japo kila moja ikiwa na kazi yake tofauti. Chembe cha moyo haswa kazi yake ni uunganishaji kwenye akili na kuhakikisha kila kitu ni shwari kwenye akili.

Akili zetu huendelea kubadilika kulingana na maswala au hali tunazokumbana nazo kimaisha. Akili za watoto huwa bado ni duni wakiwa wachanga, lakini heuendelea kunawiri pindi mtoto anvyoendelea kukumbana na hali ya kimaisha na masomo.

Akili ina sehemu nyingi zenye kazi tofauti tofauti, kuna mishipa (neurons) ambazo ni waya zinazounganisha sehemu tofauti za akili. Idadi ya waya hizo na namna vimepangwa uamua jinsi tunavyo fahamu, elewa,uhusiano,kumbuka mambo, na yale tunayojifunza.

Kila umri wa utotoni una umuhimu wake katika kupevuka kwa akili, hivyo basi hali tunazokumbana nazo kimaisha ni muhimu katika umri tofauti ili kuimarisha kila sehemu ya akili.

Mzazi ni kiungo muhimu katika ukuzaji wa akili ya mtoto.

Akili za watoto huwa na uwezo mkumbwa wa kuhisi na kushika mambo, hivyo basi ni vizuri kuwa makini na mwangalifu kwa mambo anayokubana nayo utotoni.

Uhusiano yenye upendo na iliyo na msimamo baina ya mzazi na mtoto ni kiungo muhimu sana katika kunawiri kwa akili ya mtoto.

Kukimu hali ya ukuzaji wa akili.

Kubeba watoto, kuwabembeleza, kuwaimbia na kuwaongelesha huwapa watoto hali nzuri ya kusisimua akili yao.

Wafundishe na kuwasomea vitabu hali kabla mtoto hajaanza kutambaa na kongea.

Wape nafasi tele ya marudio na mazoezi wanapopata ujuzi mpya. Ni vizuri kusisitiza mambo unavyotaka mtoto kuyajua ili kusaidia kuperusha akili ya mtoto.

Cheza na mtoto mara kwa mara.

Mpe mtoto nafasi ya kufanya mazoezi ya viungo kama, kuendesha baiskeli, kucheza mpira, kuruka na hata kukimbia.

Wape watoto moyo wakuwa na matumaini.

Kuwa na ratiba ya shughuli ya kila siku.

Wape moyo na kuwasifu watoto wanapokabiliana na hali mpya za kimaisha.

Mpe mtoto wasia unaoambatana na umri wake.

Mfundishe mtoto kukabiliana na jambo moja baada ya lingine.

Usimkosoe sana mtoto anaposhindwa kufanya jambo, bali msifu kwa jitihada zake.

Mwandae mtoto kwa mabadiliko ya siku za usoni.

Mpe mtoto nafasi ya kukabiliana na changamoto za kimaisha kwa hatua yake bila kumuharakisha.