Kuendeleza hali ya kujitegemea

Jambo muhimu katika uzazi ni kuendeleza watoto kujitengemea.

Watoto wengi hutegemea muskumo kutoka kwa wazazi wanapoendelea kukuwa, hii humsaidia mtoto kupata mbinu za kujitengemea. Ni vizuri kumweka mtoto wa kutoka umri wa miaka miwili kujiamulia mambo yake madogo madogo.

Uhuru wa kujiamulia utatengemea umri na uwezo wa mtoto. Mtoto anaweza kujitengemea katika sehemu Fulani na kushindwa katika sehemu zingine.

Si vyema kumfanyia mtoto jambo ambalo anaweza kufanya yeye mwenyewe, ingawa inachukuwa muda kumfunza mtoto kujifanyia mambo, ni vizuri kumfunza hivyo kwani hali ya kujitegemea kadri anapoendelea kukuwa.

Mbinu za kuendeleza kujitegemea

Mruhusu mtoto kujiamulia mambo madogo madogo kama vile ni nguo gani ya kuvaa wakati anapobadilisha.

Wakati mwingine kubali makosa yao na uwafunze kutokana na makosa yao.

Wape nafasi ya kujihusisha na kazi za nyumba kama vile kufagia, kutoa vumbi na hata kutandika vitanda.

Watengenezee ratiba za kazi ambazo itakuwa ikifuatwa barabara, hii pia itawasadia watoto kukumbuka kazi ambazo wamekamilisha.

Ni vizuri watoto wajue kwamba unajali hisia zao. Wape nafasi ya kuchangia mawazo yao kwa maswala inayowahusu.

Heshimu maamuzi ya mtoto unapohitajika kufanya hivyo.

Wafundishe mbinu za kukabiliana na matatizo na uwape nafasi ya kujaribu kufikiria vile wanavyoweza kusuluhisha shida zao wenyewe bila wewe kuwaambia.

Wape usaidizi wa maswala yanaoonekana magumu kwao.

Ni vizuri kuwapa moyo na kuwasifu wakati wanapojaribu kujifanyia mambo wenyewe.

Wape vitu vya kuchezea kulingana na umri wao ili waweze kujifunza kucheza pamoja kwa wakati mfupi.

Wafunze kukusanya vifaa vyao vya kucheza (doli) baada ya kumaliza kucheza.

Kwa watoto ambao wamepevuka kidogo ni vizuri kuwapa maagizo. Mfano, “Mwaweza kucheza lakini saa kumi na nusu muwe mumerudi hapa”.

Saidia mtoto kuwa na lengo na kufikia lengo lake.